Ligi Kuu Tanzania Bara | Odds Kubwa Mechi Za Leo
Mpangilio wa jumla:
Wakati
Ligi Kuu Tanzania Bara Odds Kubwa
Ligi Kuu Tanzania Bara ni ligi ya kiushindani ya juu kabisa nchini Tanzania, inasimamiwa na shirikisho la soka nchini Tanzania TFF. Ilianzishwa mwaka 1965, kipindi hicho ikijulikana kama "Ligi ya Taifa". Jina hilo lilibadilishwa kuwa "Ligi Daraja la kwanza" na tena ikabadilishwa kuwa ‘’Ligi Kuu’’ mnamo mwaka 1997.
Historia Ligi Kuu Bara
Historia ya Ligi Kuu Tanzania inaanzia mwaka 1929 ilipoanzishwa kifukara, tu kwa sababu ya mapenzi ya watu na soka wakaamua kuungana na kuanzisha michuano ya kutafuta bingwa, ingawa ni timu za Dar es Salaam pekee zilizokuwa zikishiriki wakati huo.
Kufika mwaka 1965, ilianzishwa michuano ya Klabu Bingwa Tanzania, ambayo ilikuwa inaanzia ngazi ya Wilaya, ikichezwa kwa mtindo wa mtoano, ingawa pia katika miaka miwili ya mwanzoni, timu za Dar es Salaama pekee ndizo zilizoshiriki.
Katika mfumo huo, bingwa wa kwanza ilikuwa ni klabu ya Sunderland ambayo hivi sasa inajulikana kama Simba SC ya Dar es Salaam, ambayo ilifanikiwa kutetea ubingwa wake msimu uliofuata, kabla ya kuutema kwa Cosmopolitan ya Dar es Salaam mwaka 1967.
Lakini wakati wote huo, bado Tanzania ilikuwa haijawa mwanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), hivyo Sunderland hawakuwahi kucheza michuano ya Afrika. Cosmo ingekuwa ya kwanza kucheza Klabu Bingwa Afrika mwaka 1968 kama isingejitoa, lakini kwa kujitoa kwao, Yanga ilifungua historia ya ushiriki wa klabu za Tanzania kwenye michuano ya Afrika mwaka 1969, baada ya kutwaa ubingwa wa nchi kwa mara ya kwanza mwaka 1968, kabla ya kuutetea mara nne mfululizo, katika miaka ya 1969, 1970, 1971 na 1972. Baada ya hapo, Sunderland ikiwa tayari imebadili jina na kuitwa Simba kurejesha taji lake mwaka 1973.
Simba ilishindwa kuutetea ubingwa wake msimu uliofuata mwaka 1974 baada ya kupokonywa na Yanga katika fainali ya kihistoria iliyofanyika Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza kwa kuchapwa mabao 2-1.
Mwaka 1975 Yanga iliutema ubingwa huo kwa Mseto SC ya Morogoro, iliyoweka historia ya kuwa klabu ya kwanza kutoka nje ya Dar es Salaam kutwaa ubingwa wa nchi.
Lakini Mseto ilishindwa kuteteqa taji hilo, ikapokonywa na Simba msimu uliofuata- na Wekundu wa Msimbazi walifanikiwa kutetea ubingwa huo kwa miaka mitano mfululizo, kuanzia mwaka 1976 hadi 1980.
Siri ya kutawala kwa Simba kwenye ligi hiyo kwa miaka yote hiyo ni kuyumba kwa Yanga baada ya kukumbwa na mgogoro mkubwa 1976, uliosababisha kukimbiwa na wachezaji wote nyota, hivyo kuanza upya kabisa kuunda timu.
Ni ndani ya kipindi hicho Simba iliweza kulipa kisasi cha kuchapwa mabao 5-0 na Yanga mwaka 1968, wakati nayo ilipowatandika watani wao hao wa jadi 6-0 mwaka 1977.
Juni 1, mwaka 1968 Yanga iliigaragaza Simba 5-0, mabao yake yakitiwa kimiani na Maulid
Julai 19, mwaka 1977 Simba nayo ililipa kisasi kwa kuibugiza Yanga mabao 6-0, wafungaji wakiwa ni Abdallah 'King' Kibadeni aliyetikisa nyavu mara tatu katika dakika za 10, 42 na 89, wakati mengine yalifungwa na Jumanne Hassan 'Masimenti' dakika za 60 na 73 na Selemani Sanga wa Yanga alijifunga dakika ya 20.
Kufika mwaka 1981, tayari Yanga SC ilikuwa imara tena na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara ingawa msimu uliofuata iliutema kwa Pan African.
Kuanzia mwaka 1982, mfumo wa Ligi ya Tanzania ulibadilishwa na kukawa na ligi tatu, kwanza ni Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza visiwani Zanzibar na Ligi Kuu ya Muungano.
Kwa ujumla muongo mzima wa 1980, taji la ubingwa wa Ligi Kuu Bara lilikuwa la kukoponyana, kwani Simba nayo mwaka 1985 ilipokonywa taji hilo na Yanga, ambayo nayo ililitema kwa timu mpya katika Ligi Kuu bara msimu wa 1986, Tukuyu Stars ya Mbeya.
Tukuyu nayo iliwarejeshea Yanga taji lao mwaka 1987, wakati mwaka 1988 Wagosi wa Kaya, Coastal Union ya Tanga ilijiingiza katika orodha ya timu zilizowahi kutwaa taji hilo. Mwaka 1989, Yanga ilifunga orodha ya mabingwa ya mabingwa wa muongo huo kwa kutwaa tena ubingwa wa Ligi kuu Bara.
Simba iliibuka mwaka 1990 na kutwaa ubingwa huo, ikitoka kuponea chupuchupu kushuka daraja msimu uliopita. Kupokonyana taji kuliendelea hata kwenye muongo wa 1990.
Orodha Ya Timu (7) Saba zilizochukua Ubingwa Ligi Kuu Tanzania Bara Mara nyingi Zaidi.
- Simba SC imeshinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara 21
- Yanga SC imeshinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara 28
- Mtibwa Sugar imeshinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara 2
- Mseto SC (Morogoro) imeshinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara 1
- Coastal Union imeshinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara 1
- Tukuyu Stars (Mbeya) imeshinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara 1
- Azam FC imeshinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara 1
Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/23
Ligi Kuu Tanzania Bara unaendelea Msimu wa 2022/23, huku timu zikichuana kuwania nafasi ya kwanza. Kiwango cha uchezaji kikiwa kimeongezeka, kukiwa na mechi nyingi zenye burudani ya kutosha. Mashabiki wanajitokeza kwa wingi kushabikia timu zao, na hivyo kutengeneza hali nzuri katika kila mchezo. Ushindani ni mkali, huku timu zikijitahidi kupata ushindi na kupanda kwenye msimamo wa ligi kuu bara. Msimu unapoendelea, pambano la kuwania nafasi ya kwanza linatarajiwa kupamba moto, weka mkeka wako kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania na ufurahie ushindi wenye odds kubwa kwa kila mechi msimu huu wa 2022/23.
Msimamo Ligi kuu Tanzania
Msimamo wa ligi kuu Tanzania unaendelea huku ukiwa umefikia nusu wa msimu huo, Yanga SC ikiwa inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara msimu huu wa 2022/23 ikiwa inafuatiwa na Simba SC na yenyewe ikiwa inafuatiwa na Azam FC ikishikilia nafasi ya tatu.
Mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu wanaweza kufuatilia msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kupitia Meridianbet, vile vile unaweza kubashiri mshindi wa mechi za ligi Kuu kwa kubeti mtandaoni na Meridianbet, Meridianbet ndio kampuni nambari moja inayoongoza kwa odds kubwa zenye ushindi mnomno kwa kila mechi.
Msimamo Wa Ligi Kuu NBC Tanzania 2022/23
Nafasi | Timu | Pointi/Alama |
1 | Yanga SC | 56 |
2 | Simba SC | 50 |
3 | Azam FC | 43 |
4 | Singida Big Stars | 43 |
5 | Geita Gold FC | 31 |
6 | Namungo FC | 29 |
7 | Kagera Sugar | 25 |
Ratiba Ya Ligi Kuu Tanzania
Ligi Kuu Tanzania sio ya kukosa hata mara moja, ili kufuatilia mechi za Ligi Kuu mashabiki na wapenzi wa michezo ya kubeti wanafuatilia Ligi kuu kwa kupitia Meridianbet.
Sasa unaweza kufuatilia ratiba ya ligi kuu Tanzania msimu huu 2022/23 hapa hapa Meridianbet kwa kupitia tovuti au application yetu.
Angalia ratiba kamili ya Ligi Kuu Bara msimu huu ili uweze kupanga bashiri zako mapema na kwa uhakika zaidi, fuatilia ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara ili usipitwe na odds kubwa na bomba kutoka kwenye kila mechi ya Ligi Kuu NBC.
Matokeo Ligi Kuu Bara Leo
Meridianbet ndio kampuni nambari moja Tanzania inayokupatia matokeo moja kwa moja live yakitokea uwanjani, huku ikikupa uwezo wa kufatilia matokeo ya bashiri ulizofanya kwenye beti zako. Kuwa wakwanza kujipatia ushinidi mnono kutokana na odds bomba za kila mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kuwa wakwanza kujua matokeo ya mechi zote za NBC ligi kuu Tanzania bara iwe unataka kujua matokeo ya jana, matokeo ya mechi za leo na hata mechi za juzi. Pakua application au tembelea tovuti ya Meridianbet kupata matokeo sahihi na uhakika za mechi zinazoendelea NBC Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu wa 2022/23.
Wafungaji Bora Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/23
Pata kuwajua wafungaji bora wa Ligi Kuu NBC Tanzania msimu huu wa 2022/23 kwa kupitia kurasa zetu Meridianbet. Pia unaweza kubashiri mtandaoni ni mchezaji gani atachukua tuzo ya mfungaji bora msimu wa 2022/23. Anza kubeti mtandaoni sasa na ujishindie vikubwa na odds zetu bomba kwa kila mechi na pia kwenye machaguo kama mfungaji bora.
Orodha Ya Wafungaji Bora Ligi Kuu NBC 2022/2023
- Fiston Mayele wa Yanga anamagoli 15.
- Moses Phirin wa Simba anamagoli 10.
- Saido Ntibazonkiza wa Simba anamagoli 9.
- John Bocco wa Simba anamagoli 9.
- Sixtus Sabilo wa Mbeya City anamagoli 7.
- Idrissa Mbombo wa Azam Fc anamagoli 7.
- Feisal Salum wa Yanga anamagoli 6.
Orodha Ya Watoa Pasi Za Goli (Assists) Ligi Kuu NBC Tanzania Bara
- Clatous Chama – Simba SC = 12.
- Ayoub Lyanga – Azam FC = 7.
- Saido Ntibanzonkiza – Simba = 7
- Sixtus Sabilo – Mbeya City = 6
- Mohamed Hussein – Simba SC = 5.
- Mzamiru Yassin – Simba = 5.
- Ally Ramadhani – Kagera Sugar = 4
Meridianbet inakupa uwezo wa kubashiri kwenye machaguo mbalimbali ikiwemo kubashiri mfungaji bora kwa msimu, matokeo ya mechi, magoli sahihi na mtoa assists nyingi zaidi kwenye ligi kuu Tanzania bara. Fuatilia msimu mzima wa Ligi Kuu Tanzania bara 2022/2023 na uweke bashiri yako kwa kubeti mtandaoni na Meridianbet - Odds kubwa Ushindi Mnono kwa kila mechi ya ligi kuu.