The Sri Sathya Sai Society of Tanzania

Kutoa chakula na vifaa vingine vya malazi kwa wanafunzi takribani 100 wa Tanzania wa Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko huko Dar es Salaam,Tanzania kwa miaka kumi na tano iliyopita.

Kutekeleza Huduma ya 'Wheels on Food' kwa makao mbalimbali ya watoto yatima huko Dar es Salaam mara kwa mara - Chakula safi na bora kiafya hupikwa,kusafirishwa na kuhudumiwa na Wanaojitolea wa Sai siku ya Jumapili ya kila mwezi.

Kutekeleza matibabu mbalimbali ya kitabibu,kuchangia damu na shughuli nyingine za huduma kama hizo nchini Tanzania.

BONGOFUN FOUNDATION TANZANIA

Bongofun Foundation ni kikundi cha kujitolea lililoanzishwa mwaka 2019 kinalojihusisha na kutoa misaada kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na hatarishi.

Wadau mbali mbali hutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu kama vyakula,  vifaa vya usafi, nguo, viti vya walemavu na mahitaji mbalimbali ya kibinaadamu kwa Watoto yatima. Bongofu huwakilisha sehemu husika kutoa  misaada hiyo.

Kama mmoja ya wadau wanaounga mkono kikundi hichi katika kuhakikisha kila mtoto anayeishi katika mazingira yanayostahili, unaweza kuchangia sasa.

Bongofun Foundation, Mtoto wa mwenzio ni wako!

CCP Medicine

CCPMedicine Medical Center ni Taasisi ya Kinga Dhidi ya Magonjwa Sugu (The Community Center for Preventive MedicineCCPmedicine) ilisajiliwa rasmi mwaka 2013. 

Watu wengi wanaopata magonjwa sugu kama presha, kisukari, pumu, macho, meno na saratani za; matiti, mlango wa kizazi, tezi dume, koo, tumbo na utumbo hufika hospitali huku wameshachelewa na athari zinaonekana. 

Taasisi hii inafanya kazi ya kuwafikishia watu huduma ya kinga daraja la kwanza sehemu wanayoishi. Huduma Zitolewazo; 
- Udhibiti magonjwa sugu kupitia vipimo, tiba na ushauri,
- Huduma kwa makundi maalumuWazee|Wastaafu
- Tiba Shufaa-“Palliative Care”
- Huduma za wagonjwa majumbani, maofisini na walio safarini
- Kinga daraja la pili, na tatu-“Rehabilitation Health Services”

Tafadhali karibu kuchangia ili huduma hii iwafikie watu wengi zaidi na kuokoa maisha!